Kuhusu FINCA
FINCA Microfinance Bank Limited Tanzania ni moja ya waanzilishi kongwe wa masuala ya kifedha. Kupitia uzoefu kongwe wa miaka mingi na kuungwa mkono na mtandao wa kimataifa, tunatoa ujuzi unaosaidia wateja wetu kutimiza malengo yao ya kifedha na kutengeneza malengo bora ya baadaye.
FINCA Microfinance Bank Limited Tanzania tunawawezesha wateja kwa kuwapa bidhaa, huduma na elimu itakayowawezesha kuboresha kiwango cha maisha, kutengeneza mazingira bora ya kifedha na udhibiti, na kusomesha watoto wao shule.
FINCA ilianzisha Benki yake ya kwanza ya Kijiji huko Mwanza mnamo mwaka 1998, na kuleta chachu ya ukopeshwaji wa vikundi nchini Tanzania. Kuanzia hapo, Zaidi ya wateja milioni moja wameweza kupata huduma za kifedha ikiwa ni pamoja mikopo, kuweka akiba pamoja na kufanya miamala.
Kama kiongozi katika masuala ya fedha, tulikuwa taasisi ya kwanza ya mikopo midogo midogo kupewa leseni na Benki Kuu ya Tanzania, leseni iliyotuwezesha kutoa huduma za kibenki na kuchukua amana kutoka kwa umma. Kupitia Ubunifu kama vile wakala na huduma za kibenki kwa njia ya simu imerahisisha zaidi utekelezwaji wa miamala. Kwa muda wa dakika tano, mteja anaweza kufungua akaunti ya akiba kwa kutumia kompyuta au simu kupitia mfumo wetu wa kidigitali.
Kwa siku zijazo, tunatengeneza na kurahisisha michakato yetu ya mikopo na huduma kwa wateja ili kuboresha zaidi huduma zetu huku tukidumisha ahadi yetu ya kutoa huduma za kipekee kwa wateja.

