AKAUNTI YA MIPANGO (AKAUNTI YA KIASI NA MUDA MAALUMU AMBAYO INAKUFANYA UPATE FAIDA YA HADI ASILIMIA 14)

Je, una biashara au lengo binafsi ambalo ungependa kufanikisha ndani ya kipindi cha muda maalumu? Akaunti ya Mipango inakusaidia kujenga njia imara ya kufikia ndoto zako na kuondoa mwanya kati ya mipango na mafanikio yako. Njoo uweke fedha zako FINCA na upate faida ya hadi asilimia 14.

  • Uhuru ni wa kwako, anza kuweka akiba kuanzia miezi 3 hadi mwaka 1 kwa kianzio cha salio la TZS 50,000 tu

  • Hakuna ada za uendeshaji wa akaunti

  • Unaweza kuongezea kiasi chako cha awali wakati wowote na kuweza kuongeza faida yako kwa kuzingatia kiwango cha siku ya nyongeza

  • Kuweza kuonana na Meneja Uhusiano na kumfanya awe mlezi wako atakayetatua matatizo yoyote yanayokukabili

  • Mchakato wa kufungua akaunti wa haraka na usio na usumbufu

  • Upataji wa Mkopo wa FINCA kwa urahisi