MFUMO WA MALIPO BAINA YA BENKI TANZANIA (TISS)

Mfumo wa Uhamishaji wa Fedha (RTGS) ulifungwa na Benki Kuu ya Tanzania. Huu ni mfumo wa mtandaoni ambao unawezesha maelekezo ya malipo kufanyika kikamilifu na kwa muda mfupi baina ya benki mbalimbali.
Ufanyaji kazi wa TISS unajumuisha usimamizi wa Akaunti mtandaoni na miamala ya uhamishaji wa fedha za thamani kubwa baina ya benki au uhamishaji wa fedha kwa kuzingatia muda. TISS unaongeza ufanisi katika mfumo wa malipo kwa kuondoa ucheleweshaji wa malipo makubwa na kuzingatia muda. Pia TISS unapunguza hatari za upotevu wa fedha.

FAIDA

  • Pata huduma za malipo zenye ufanisi na zinazofaa kwa wasambazaji wako au mtu aliyekusudiwa katika Muda Mwafaka.
  • Salama kwa kuwa inadhibitiwa, ilianzishwa na kusimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania.

MONEYGRAM

Kutuma na kupoka fedha nchini na kimataifa kwa sasa ni rahisi Zaidi kwa kutumia FINCA Microfinance kwa kuwa tunaungana na MoneyGram kukupa nguvu ya kuhamisha fedha katika Matawi zaidi ya 20 Tanzania nzima. Tembelea Matawi yetu na upate huduma katika Kaunta zinazotoa huduma.