Nafasi za kazi

Angalia Fursa za Ajira kutoka FINCA Tanzania.

Ni zaidi ya kazi

FINCA ina dhamira kabambe ya kumaliza umaskini. Ili kuendeleza dhamira hiyo, tunategemea nguvu kazi ya kimataifa ya wafanyakazi 7,000 wenye vipaji waliojikita kuwawezesha watu wenye ndoto na malengo ya kuwa na maisha bora ya baadae.

Kwa pamoja, tunatoa ufikiaji wa bidhaa, huduma na elimu ambayo huwasaidia wateja kuanzisha au kukuza biashara, kuweka akiba kwa ajili ya siku zijazo na kusomesha watoto wao shuleni. Tunawasaidia kujenga uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na majanga mengine. Matokeo ya haya yote tunayaona kwenye maisha ya wateja wetu

Maono ya kiulimwengu, moyo wa jamii yetu

Kama shirika la kimataifa, wafanyakazi hunufaika kutokana na kupata mbinu bora za sekta na mara nyingi huwa na fursa za kushirikiana na wafanyakazi wenzao duniani kote. Lakini kazi kubwa na muhimu zaidi inafanywa wafanyakazi wa Tanzania. Wafanyakazi wengi wanaishi na kufanya kazi katika jumuiya wanazohudumia. Tunazingatia tamaduni na mitazamo ya wenyeji na kujitolea katika kusimamia na kumiliki biashara hii.

Maadili Yetu

Wafanyikazi wetu wanaonyesha kuguswa, huduma, usikivu wa dhati, uwajibikaji, heshima, sifa za chapa yetu ambazo ni uchangamfu, uaminifu, na uwajibikaji wa benki. Tunazingatia teknolojia na uvumbuzi ili kuongeza ubora wa kuwahudumia vyema wateja wetu.

Jiunge na Timu Yetu

Tunakaribisha watahiniwa wenye taaluma tofauti tofauti. Tunatafuta watu ambao tunaweza kujenga nao uhusiano thabiti na wa kudumu – watu wanaojali, na wanaoheshimu, wateja. Tunatafuta wenzetu watakaofanya kazi zao kwa furaha, uvumbuzi, na hali ya kufanya kwa ziada.

Nafasi Mpya za Kazi

Tazama hapa chini nafasi za kazi na kazi za intenship

Nafasi za kazi zinapatikana kwa lugha ya Kiingereza pekee. Tafadhali tazama hapa.