Ulinzi taarifa za wateja
Ni kipaumbele kikubwa cha FINCA Tanzania kuzingatia mahitaji ya wateja, maoni na kutoa majibu kwa kila jambo litakaloulizwa. Wateja wetu ni wa kipekee na lengo letu kubwa ni kuhakikisha sauti zao na maoni yao yanasikika.
FINCA Tanzania inaongozwa na lengo kuu la kutanguliza maslahi ya wateja wetu na kufuata mara kwa mara kanuni za ulinzi wa mteja zilizoidhinishwa katika sekta ya huduma za kifedha. Tunathamini uhusiano wa muda mrefu na thabiti kuwahudumia wateja kwa bashasha, uaminifu na uwajibikaji.
Tunatii kila Kanuni ya Ulinzi wa Mteja ili kuhakikisha kwamba tunatoa bidhaa zinazofaa kwa wateja wetu, kuchukua hatua ili kudhibiti madeni kupita kiasi kwa wateja wetu, pamoja na kwamba sheria, masharti na bei zetu ni za uwazi tunalinda taarifa ya faragha ya mteja kwa kutumia mbinu zote kujibu maswali na hoja za mteja.
Tunawahimiza washikadau wote (ikiwa ni pamoja na wafanyakazi, wanahisa, wateja, watoa huduma na wadhibiti) kufichua matukio yote yanayowezekana au yanayoshukiwa kuwa ya utovu wa nidhamu.
Maoni, mapendekezo au malalamiko yako yanaweza kuwasilishwa kupitia njia zifuatazo:
- Piga Simu: +255 (0) 755 980 350
- Tuma barua pepe kwenda: [email protected]
Jaza fomu
Kumbuka: Barua, simu na barua pepe zinashughulikiwa kwa uangalifu na usiri na FINCA Tanzania.

