Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara (kama hutapata jibu la swali lako hapa, usisite kupiga simu katika Kituo chetu cha Kupokelea Simu kwa Namba 0755980350 au tuma baruapepe kupitia info@fincatz.org)

FINCA Microfinance Bank inatoa masuluhisho kamili ya kifedha yanayotokana na mahitaji ya wateja wetu. Hayo yanajumuisha Akaunti za Akiba, Masuluhisho ya Mkopo, Akaunti za Amana za Muda Maalumu, Akaunti za Miamala, Masuluhisho ya kuhamisha Fedha, Masuluhisho ya Malipo na Usimamizi wa Mshahara kwa mtu hadi katika ngazi ya shirika. Utoaji wetu ni wa viwango vya ushindani, njia za upatikanaji kidijiti na usalama wa miamala.

FINCA Microfinance Bank inatoa njia ya gharama nafuu, rahisi na salama ya kupata fedha zako kupitia matawi zaidi ya 20 yaliyopo Tanzania, mtandao wetu wa wakala (FINCA Express Wakala) tukiwa na vituo zaidi ya 150 vinavyopatikana karibu na biashara yako au nyumbani na kupitia huduma za benki mtandaoni (piga *150*19#).

FINCA Microfinance Bank inatoa uzoefu wa hali ya juu kwa wateja wetu, ikijumuisha kujibu maswali na maombi yote. Wateja wetu wanaweza kutufikia katika tawi lolote. Kwa kupitia njia za kidijiti, benki inaweza kufikiwa kupitia anwani ya info@fincatz.org au kwa kupiga simu katika Kituo Chetu cha Kupokelea Simu kwa namba isiyo na malipo ya 0755980350.

Benki inatoa akaunti mbalimbali za akiba zinazowawezesha wateja wetu kupanga kwa ajili ya siku zijazo. Akaunti zilizopo ni pamoja na Akaunti za Mipango (Mipango Standard na Mipango Pay-out) ambazo zinawawezesha wateja kupata riba kwa muda maalumu wa miezi mitatu. Akaunti ya Hakika (Hakika Account) pia inaruhusu wateja kupata riba lakini kwa uwezo wa kuchukua pesa mara moja kwa mwezi bila malipo. FINCA pia inatoa Akaunti ya Mkwanja (Mkwanja Account), akaunti ya miamala inayowawezesha wateja kufanya miamala ya kila siku kwa mahitaji yao.

Masuluhisho yetu ya mkopo yanatolewa kwa Mtu binafsi hadi Mikopo ya Kikundi. Mikopo ya Mtu Binafsi inajumuisha Mkopo wa Biashara, Mkopo wa Ada ya Shule, Mkopo wa Biashara Ndogondogo na Mkopo kwa Wanaotoa Huduma ya Elimu. Aina za Mikopo ya Kikundi zinajumuisha Mikopo ya Pamoja (Pamoja Plus) na Mkopo wa Kikundi cha Kijamii (Social Financial Group Loan).

Kwa miaka mingi FINCA Microfinance Bank imekuwa ikiongoza katika tasnia ya taasisi ndogo za fedha kutokana na uwezo wake wa kuwahudumia wateja kwa haraka na kwa urahisi. Mikopo inaweza kutolewa ndani ya siku tatu au pungufu kutokana na Kutumia Njia ya Kiotomati ya Digiti (Digital Field Automation (DFA)) ambayo inawawezesha Maofisa wa Uhisiano na Wateja kupokea na kupitisha fomu za data za maombi ya mikopo ugani –nyumbani kwa mteja au mahali pa biashara.

Kiasi chako cha malipo ya kila mwezi kitategemeana na kipindi kilichothibitishwa cha mkopo na kiasi cha mkopo.

Viwango vyetu vya mkopo vinaanzia TSH.200,000 hadi TSH.milioni 220 kutegemeana na aina ya mkopo na uwezo wa mkopaji

Ndiyo. Mkopo wa Elimu unalipwa moja kwa moja katika taasisi ya elimu na unaweza kupatikana hata kama mkopaji analipa mkopo mwingine.

Mawakala wa FINCA

Gharama ni kwenye gharama za kutoa fedha tu. Kiasi kinachotozwa kwa kila muamala wa kutoa fedha ni TZS 590

Go to Top