FINCA Microfinance Bank nchini Tanzania ilikuwa ni taasisi ndogo ya kwanza ya fedha nchini iliyopewa leseni na Benki Kuu ya Tanzania. FINCA Microfinance Bank ni sehemu ya mtandao wa dunia wa FINCA Impact Finance wa benki 20 na taasisi ndogo za fedha ambazo zinatoa huduma za fedha zinazoleta mabadiliko na kuwajibika katika jamii zinazowawezesha watu wenye kipato cha chini kuwekeza kwa ajili ya mustakabali wao.

Pamoja na uzoefu wa miaka zaidi ya 30 na kuwa na wafanyakazi wazawa wengi zaidi ya 10,000, FINCA Impact Finance inatoa faida kubwa ya uendelevu ya kibishara na matokeo mazuri ya kijamii.

HATUA MUHIMU

1985 – Kuanzishwa kwa FINCA International
Msingi wa Msaada wa Kimataifa kwa Jamii (FINCA) ulianzishwa

1998 – Kuanzishwa kwa FINCA Tanzania
FINCA Tanzania ilizinduliwa na kuanza kutoa huduma za fedha

2012 – Mabadiliko ya FINCA Tanzania M.F.C Limited
FINCA Tanzania ilikuwa taasisi ndogo ya fedha ya kwanza kupewa leseni na Benki Kuu ya Tanzania, ikawa FINCA Tanzania M.F.C Limited.

2013 – Mabadiliko kuwa Taasisi Inayotoa huduma za Kibenki
FINCA Tanzania imeruhusiwa kisheria kutoa huduma za benki na Benki Kuu ya Tanzania

2014 – Kuzinduliwa kwa FINCA Express (Agency Banking)
2014 – Mabadiliko kutoka FINCA Tanzania M.F.C Ltd kuwa FINCA Microfinance Bank

2015 – FINCA Tanzania kuwa benki inayotoa huduma kamili
Baada ya miaka 17 ya uendeshaji kama taasisi ndogo ya fedha, FINCA Tanzania inafungua ukurasa mpya kama benki inayotoa hudumakamili

2018 – FINCA Microfinance Bank inafikisha miaka 20 ya kutoa huduma za fedha na kuwawezesha wasiotumia huduma za benki 
Kwa miaka 20 ya uendeshaji nchini Tanzania, FINCA Microfinance Bank inaendelea kuongoza katika tasnia ya benki — ikitoa masuluhisho ya fedha kidijiti na bidhaa na huduma za fedha zinazofaa: Akaunti za Akiba na Miamala; Mikopo, Masuluhisho ya Malipo; na Akaunti za Muda Maalumu.

HISTORIA YETU KWA UFUPI

UBUNIFU NI MUHIMU