Matarajio
Wateja wetu ndio lengo la kila kitu tunachofanya. Wanapofanikiwa, tunafanikiwa.
FINCA iko mstari wa mbele katika ubunifu na masuala ya kifedha, kuweka viwango bora kwa ajili ya sekta ya mikopo midogo midogo na kutengeneza bidhaa na huduma mpya zinazowasaidia wateja wetu kufikia ndoto zao. Tunaweka msukumo kwenye mahitaji na matarajio yao kupitia uhusiano mzuri wa wateja na mpango thabiti wa tafiti. Sifa ya chapa yetu ya uchangamfu, uaminifu, na uwajibikaji wa benki huonekana kwa kila huduma itolewayo kwa wateja.
FINCA Kimahesabu
Ulimwenguni kote, FINCA inawezesha kifedha maisha ya watu milioni 3.4 kila mwaka. Nchini Tanzania, FINCA imehudumia zaidi ya wateja milioni moja tangu mwaka 1998.
Kufikia watu wasiohudumiwa
FINCA Microfinance Bank Limited Tanzania inatoa huduma maalum kwa wanawake na watu kutoka vijijini, kwa kutambua yakwamba hawapati kwa urahisi huduma kutoka taasisi za fedha.
Elimu kwa Mteja
FINCA inapotoa elimu ya kifedha pamoja na mikopo na huduma za kuweka akiba, wateja wetu hufanikiwa zaidi. Tunatoa elimu bure ya kifedha na kiufundi kuhusu mada mbalimbali kama vile bajeti ya msingi, mipango ya kifedha, maendeleo ya kilimo na ujasiriamali. Matoleo haya ya elimu ya kifedha yanawawezesha hasa wanawake na makundi mengine ambayo kihistoria yanashindwa kupata usawa wa rasilimali hizo.
Huduma kwa Jamii zetu
Kwa kuzingatia dhamira yetu ya kujenga kesho bora kwa wateja wetu, tunajivunia kuwekeza muda na vipaji vyetu kwa manufaa ya jamii zetu. Tumelenga kufikia shughuli zinazosaidia wateja wetu na mifumo yao ya maisha.

