Wawekezaji na Washirika
Wawekezaji na washirika wa FINCA Microfinance Bank Limited Tanzania wanaunga mkono dhamira yetu kwa kutoa rasilimali muhimu ili kusaidia kupunguza na kuondoa umasikini Duniani.
FINCA Microfinance Bank Limited Tanzania inafanya kazi na wawekezaji na washirika wengi ili kuongeza uwezo wake wa kuleta ushirikishwaji wa kifedha kwa watu wengi zaidi. Ushirikiano huu pia unasaidia FINCA kujenga miundombinu muhimu ili kuboresha uzoefu wa wateja kupitia teknolojia huku ikidumisha uhusiano wa wateja kwa bashasha na uaminifu ambao ni alama mahususi ya chapa ya FINCA.
FINCA Microfinance Bank Limited Tanzania ni kampuni tanzu ya FINCA Microfinance Holding Company LLC (FMH) uwekezaji wa kijamii (SRI) ambao unamiliki na kuendesha taasisi ndogo za fedha na benki duniani kote. Wawekezaji wa FMH wanaongozwa na FINCA International Inc. shirika lisilo la kifaida lenye makao makuu Washington, D.C.- na wanahisa wengi wa FMH. Wanahisa wachache wa FMH ni Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC), KfW, Nederlandse Financierings-Maatschappij voor Ontwikkelingslanden N.V. (FMO), Triple Jump na Triodos. Pata maelezo zaidi kuhusu wanahisa wa FMH.

