Beatus Malawa
Mkuu wa masuala ya Sheria, Uzingatiaji na Katibu wa Kampuni
Beatus Malawa ni wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 7 katika kushauri mashirika katika masuala ya kibenki na fedha, sheria ya mashirika na biashara, na mashauri ya madai.
Beatus ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria, Uzingatiaji na Katibu wa Kampuni wa FINCA Tanzania, vilevile ni mjumbe wa Bodi ya Menejimenti yenye dhamana ya kusimamia shughuli za kisheria za FINCA Tanzania na utawala bora wa shirika. Ana kaimu kama Katibu wa Bodi ya Wakurugenzi na Kamati ya Bodi ya FINCA Tanzania.
Kabla ya kujiunga na FINCA Tanzania, Beatus alifanya kazi katika kampuni ya uwakili ambapo alianza kama Afisa Sheria na AccessBank Tanzania Limited na kukua hadi Afisa Mwandamizi wa Sheria. Kisha alijiunga na FINCA Tanzania kama Wakili Mwandamizi wa Kisheria na baadaye akawa Mkuu wa Sheria, Uzingatiaji na Katibu wa Kampuni.
Beatus Malawa ana shahada ya kwanza ya sheria kutoka Chuo Kikuu cha Tumaini, Iringa. Pia alipata shahada ya uzamili ya sheria kutoka Shule ya Sheria ya Tanzania.


