Felician Leonce Girambo
Afisa Mkuu wa Biashara
Kama Afisa Mkuu wa Biashara, Felician ni memba wa Bodi Kuu ya Usimamizi inayohusika na kukuza mali na madeni ya benki kupitia mtandao wa matawi na njia nyingine za utoaji huduma. Anaongoza maendeleo na utekelezaji wa mkakati wa upanuzi unaoiwezesha FINCA Microfinance Bank (“FINCA Tanzania”) kufikia malengo yake ya kuwafikia wateja. Aidha, kama memba wa Timu ya Usimamizi wa Utendaji, anashiriki jukumu la utendaji wa jumla na shughuli za FINCA Tanzania na kushiriki katika kufanya maamuzi kuhusu masuala muhimu.
Felician analeta uzoefu mkubwa katika hatari za mikopo na benki za biashara. Katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, amefanya kazi katika benki kadhaa katika nyadhifa tofauti ikiwemo Mkuu wa Mikopo, Benki ya Watu Binafsi na Biashara katika Stanbic Bank Tanzania Limited, Mkurugenzi wa Biashara Akiba Commercial Bank, Mkuu wa Ujumuishaji wa Kifedha Letshego Bank Tanzania, Afisa Mkuu wa Mikopo DCB Commercial Bank Plc Tanzania, Afisa Mwandamizi wa Mikopo NMB Bank na Mchambuzi wa Mikopo katika CRDB Bank Plc.
Felician ana shahada ya Uzamili (MSc) katika masuala ya fedha kutoka Chuo Kikuu cha Strathclyde, diploma ya uzamili katika usimamizi wa kifedha kutoka Maastricht School of Management nchini Uholanzi, na shahada ya Biashara (BCom) katika masuala ya fedha kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Felician pia amehudhuria mafunzo kadhaa ya kimataifa ikiwemo mafunzo ya usimamizi wa hatari za biashara kutoka SIDA huko Stockholm, Uswidi pamoja na mafunzo ya uongozi katika fedha jumuishi kutoka Harvard Business School huko Boston, Massachusetts, Marekani.


