Isaack Chahe

Afisa Mkuu wa Fedha

Akiwa kama Afisa Mkuu wa Fedha, Isaack anaongoza Idara ya Fedha na Utawala ya FINCA Tanzania. Anawajibika kusimamia shughuli zote za kifedha, uhasibu na utawala, na pia anasimamia wafanyakazi wa idara hizo. Anahakikisha kuwa shughuli za fedha na utawala zinaisaidia FINCA Tanzania kutimiza malengo yake  na kwa ufanisi mkubwa.

Kama mmoja wa timu ya menejimenti ya FINCA/Bodi, anahusika kwenye jukumu la kusimamia utendaji wa jumla na shughuli za FINCA Tanzania, na hushiriki katika kufanya maamuzi juu ya masuala muhimu.

Isaack alijiunga na FINCA akiwa na uzoefu wa zaidi ya miaka ishirini na mitano katika sekta za benki na fedha. Alianza taaluma yake katika Benki ya Standard Chartered Tanzania kama Afisa wa Uhasibu (2000–2005), kisha akafanya kazi na African Banking Corporation, Kenya Commercial Bank (Tanzania), ECO Bank, Mwanga Hakika Bank, Letshego Bank Tanzania Ltd, na Letshego Faidika Bank, akihudumu katika nyadhifa mbalimbali kuanzia Meneja wa Fedha na Utawala hadi Afisa Mkuu wa Fedha.

Isaack ni Mhasibu wa Umma aliyeidhinishwa (CPA-T) tangu mwaka 2004 na ana shahada ya BCom (Hons) katika Biashara na Usimamizi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Amehudhuria mafunzo mbalimbali ya kitaaluma katika nyanja za uhasibu, fedha, usimamizi wa biashara na uongozi