Jeffrey Smith
Makamu wa Rais na Afisa Mkuu Tawala
Jeffrey Smith ana uzoefu wa takriban miaka 45 katika ukaguzi, fedha, uhasibu, usimamizi salama, udhibiti wa ndani, uzingatiaji wa kanuni, rasilimali watu, teknolojia, usalama wa habari na mwendelezo wa biashara. Ameongoza juhudi nyingi za maboresho, pamoja na juhudi nyingi za kimataifa katika kutekeleza udhibiti madhubuti wa kifedha, kuzuia utapeli na mifumo angalizi ya ufuatiliaji.
Bwana Smith amefanya kazi katika sekta za umma na binafsi na amekuwa mshauri wa kujitegemea na kushika nyadhifa za kimataifa katika Citibank na kampuni ya Ford Motor na Rotary International.
Bw. Smith ni Mtaalam wa masuala hatarishi ya kifedha aliyeidhinishwa na alipata Shahada ya Uzamili ya Utawala wa Biashara kutoka Chuo Kikuu cha Wayne State (Detroit, Michigan, Marekani) na Shahada ya Kwanza ya Utawala wa Biashara kutoka Chuo Kikuu cha Eastern Michigan (Ypsilanti, Michigan, Marekani).


