Muhammad Siddique Ahmed
Mjumbe wa Bodi
Muhammad Siddique Ahmed ana uzoefu wa Zaidi ya miaka 22 katika usimamizi mkuu katika nyanja ya masuala ya Fedha, Ukaguzi na Uchunguzi wa utapeli. Akiwa amefanya kazi Marekani na nchi kadhaa barani Afrika na Asia, ana ujuzi na utaalamu wa kina katika masuala ya benki, mikopo midogo na fintech. Kwa sasa Bwana Ahmed anafanya kazi kama Mkaguzi Mkuu wa Ndani katika Mobilink Microfinance Bank Ltd, Benki kubwa zaidi ya kidijitali nchini Pakistan. Kabla ya kufanya kazi Mobilink, Bwana Ahmed aliwahi kuwa Mkuu wa Ukaguzi wa Ndani katika Benki ya HBL Microfinance. Kabla ya HBL, Bw. Ahmed alifanya kazi kama Mkaguzi wa Ndani wa Kikanda wa FINCA Microfinance Holding (FMH) na alihudumu katika kanda za Afrika, Mashariki ya Kati na Kusini mwa Asia. Bwana Ahmed amebobea katika utawala, usimamizi wa masuala hatarishi ya kifedha, utekeleaji, fedha na ukaguzi.


