Pamoja Loan: Kuziwezesha biashara ndogondogo na jamii kwa ujumla

Pamoja loan ni mkopo wa kikundi kutoka benki ya FINCA wenye lengo la kuwawezesha wamiliki wa biashara ndogo ndogo ambao wameshindwa kufikiwa na huduma za kibenki.

Sifa na Faida
  • Muundo wa kupata mkopo kwa kikundi Inabidi kujiunga kwenye kikundi cha wajasiriamali wasiopungua 10. Hii inasaidia kusaidia wajasiriamali wengi kwa pamoja na kupunguza hatari kwa mkopeshaji kwa sababu wajasirimali hawa wanafahamiana zaidi.

  • Kiasi cha Mkopo Unachoweza Kukopa
    Kiasi cha mkopo kinaanzia TZS 100,000 hadi TZS 5,000,000 kwa kila mwanakikundi lakini mtu mmoja hawezi kukopa zaidi ya 35% ya mkopo wote wa kikundi. Mkopo unatolewa kwa mahitaji madogo dogo ya biashara na kukuza mtaji.

  • Masharti Rahisi ya Ulipaji
    Yametengenezwa masharti rahisi ya urejeshaji wa mkopo ili kuendana na mzunguko, mtiririko wa pesa wa biashara ndogo ndogo na chaguzi za malipo ya kila wiki, kila wiki mbili au kila mwezi.

  • Kujenga Uwezo
    FINCA Tanzania inatoa mafunzo ya ujuzi wa masuala ya kifedha na maendeleo ya biashara kwa wateja wa mkopo wa Pamoja. Lengo ni kuwapa ujuzi unaohitajika wafanyabiashara hawa wadogo ili kusimamia fedha zao kwa ufanisi na kukuza biashara zao.

  • Mahitaji ya Dhamana ya nafuu
    Muundo wa mkopo wa kikundi unawasaidia wajasiriamali wadogo kupata mkopo kwa dhamana nafuu zilizo ndani ya uwezo wao.

Tukue Pamoja : Pata Mkopo Wako Sasa!

Je, unataka kufahamu zaidi kuhusu bidhaa zetu nyingine za mikopo vikundi: bonyeza hapa kwa mkopo ya Bajaji na mkopo wa Sokoni ili kujua zaidi!