Je unajua Jinsi ya kupanga Bajeti?

Bajeti ni mpango unaouandaa ili kuamua jinsi utakavyotumia pesa zako kwa muda fulani (kila siku, wiki, mwezi, mwaka) na mpango huu unakuonyesha: ni kiasi gani cha pesa unachotengeneza na jinsi unavyotumia.

Kupanga Bajeti ni rahisi kama hivi:
  • Andaa bajeti kwa kukusanya bili zako na andaa jedwali la matumizi yote: fikiria jinsi unavyotumia pesa, mbali na unavyolipia bili zako. Kwa mfano, Je unanunua kikombe cha kahawa kila siku? Je, unalipia elimu, burudani? Baada ya mwezi mmoja, pesa ulizotumia kwenye kahawa, elimu na burudani zinaweza kuongeza gharama, hizo unaweza kuziandika.

  • Unapokuwa na bili zako na kuandaa jedwali la matumizi: andika gharama zako (pesa unazotumia).

  • Andika ni kiasi gani cha pesa unachotengeneza: kwa maneno mengine: mapato yako ni nini.

  • Ondoa matumizi yako kutoka kwa kiasi gani cha pesa unachotengeneza.

  • Kama namba ni chini ya sifuri: unatumia pesa nyingi kuliko unazopata. Angalia ni vitu gani kwenye bajeti yako unaweza kuvibadilisha. Labda kuna baadhi ya vitu huviitaji, na kuna njia ya kutumia hela kidogo zaidi