22-04-2026
Nguvu ya Ushindi: FINCA Yashinda Medali katika Mbio za Kilimanjaro 2026
Mapema mwaka huu Benki ya FINCA ilishiriki kwa fahari kubwa kwenye Mashindano ya Kimataifa ya Mbio za Kilimanjaro 2026, mbio zaa kila mwaka zinazofanyika mkoani Kilimanjaro.
Timu yetu iliongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Felician Girambo,hali iliyotoa morali ya hali ya juu na kufanikisha ushindi wa medali kadhaa katika mbio za kilomita 21.
Ushindi huu unaonyesha nguvu ya mshikamano miongoni mwa wafanyakazi, nidhamu, na dhamira yetu ya pamoja ya kufanikisha ubora ndani na nje ya kazi.
Tukiongozwa na kaulimbiu ya mwaka huu, “Kila kona, kila hatua, kwa kasi zaidi,” tunaendelea kuvuka mipaka na kujitahidi kufikia mafanikio makubwa zaidi.



