19-06-2024

Benki ya FINCA Yafungua Ofisi Mafinga ili Kuwafikia Wajasiriamali Wengi Zaidi

Benki ya FINCA Tanzania inayo furaha kutangaza ufunguzi wa ofisi yake mpya huko Mafinga iliyoko karibu na soko la Mafinga. Mafinga ina idadi inayokua ya watu na muhimili wa kibiashara unaochipukia kwa kasi.

Mafinga ni eneo ambalo Kuna fursa za maendeleo ya kibiashara zikiwemo ndogo na za kati (SMEs) katika sekta mbalimbali. Fursa hizi ni pamoja na kilimo biashara, huduma za utalii na biashara ya rejareja.

Kwa kuwasaidia wafanyabiashara wadogo na wa kati kupitia ufikiaji wa huduma za kifedha, huduma za maendeleo ya biashara, na mnyororo wa masoko kunaweza kukuza ukuaji wa kiuchumi na kutengeneza ajira katika eneo hilo, hili ndio lengo kuu la benki ya FINCA. Ukuaji huu unawakilisha hatua muhimu katika ahadi ya FINCA ya kutumikia vizuri wateja wake na jamii kwa ujumla.

Ofisi hii mpya ya FINCA inakusudia kuhakikisha na kukuza uzoefu wa kibenki na wa urahisi wa huduma kwa wateja wake wote. Ndani ya ofisi hii wateja wataweza kufungua akaunti, kuomba mikopo au kupata ushauri wa kifedha kutoka kwa timu ya wataalamu wa FINCA ambao wako tayari kusaidia wateja katika kila hatua.

FINCA Tanzania inaamini katika kujenga uhusiano imara na wateja, na ofisi impya inawezesha FINCA kuimarisha zaidi uwepo wake na msaada ndani ya Mafinga.