15-05-2025

FINCA Tanzania yashiriki Kilimanjaro International Marathon 2025

Kama sehemu ya kuunga juhudi za kuisaidia jamii inayoihudumia, FINCA Tanzania mapema mwaka huu ilishiriki Mbio za Kimataifa za Kilimanjaro za mwaka 2025.
Kwa ushiriki huo FINCA ilichangia kampeni ya “Tumaini la maisha” ambapo waandaaji wa mbio hizo walitoa 5% ya kila ada ya ushiriki kusaidia matibabu ya watoto wanaougua saratani.
Washiriki kutoka FINCA walivalia mavazi yenye nembo ya “FINCA Runners” ambayo pia ilisaidia kwa nembo ya FINCA kuonekana kwa zaidi ya washirki 20,000 katika mbio hizo.
Pongezi za dhati kwa Afisa Mkuu wa Biashara, Felician Girambo, ambaye alipata medali kwa kumaliza mbio za kilomita 21 kwa wakati.