15-05-2025

Msaada kwa Wafungwa Wanawake Gereza la Segerea

Katika kuadhimisha siku ya wanawake Duniani, Wanawake kutoka benki ya FINCA walipata wasaa wa kutembelea gereza la wanawake Segerea. Hii ilikuwa ni fursa ya kipekee kwa wanawake wa FINCA kuungana na kusaidia wanawake wenzao.
Walipeleka mahitaji mbalimbali kwa wafungwa hawa wa gereza la Segerea. Mahitaji haya yalijumuisha vitu muhimu kama vile Sabuni, dippers za watoto, mafuta, nguo, na taulo za kike,n.k. Hii ikiwa ni msaada wa vitu kwa ajili ya matumizi mbalimbali katika maisha yao ya kila siku.
Lengo la FINCA ni kuendelea kuigusa jamii na kuleta tabasamu kwa watu wenye changamoto na kuharakisha jitihada zao za kuboresha maisha yao.
Kama sehemu ya kuadhimisha hashtag#IWD2025, tunasisitiza kwamba “Accelerate Action” – tuharakishe hatua kwa manufaa ya jamii, kwa maendeleo ya wanawake na watoto, na kwa mustakabali bora wa Taifa letu.