habari na matukio
Jifunze habari za hivi punde kuhusu FINCA Tanzania na kazi zetu katika jamii.
Maswali ya Vyombo vya Habari: [email protected]
News 06-05-2026
Katika ziara yake ya hivi karibuni nchini Tanzania, Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Benki za FINCA, Andrée Simon, alitembelea Soko la Kariakoo ili kukutana na wafanyabiashara na wateja wa eneo hilo.
News 23-04-2026
Tunafurahi kutangaza uteuzi wa Dru Jayaratne kuwa Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa FINCA Tanzania.
News 22-04-2026
Mapema mwaka huu Benki ya FINCA ilishiriki kwa fahari kubwa kwenye Mashindano ya Kimataifa ya Mbio za Kilimanjaro 2026, mbio zaa kila mwaka zinazofanyika mkoani Kilimanjaro.
News 15-05-2025
Katika kuadhimisha siku ya wanawake Duniani, Wanawake kutoka benki ya FINCA walipata wasaa wa kutembelea gereza la wanawake Segerea. Hii ilikuwa ni fursa ya kipekee kwa wanawake wa FINCA kuungana na kusaidia wanawake wenzao. Walipeleka mahitaji mbalimbali kwa wafungwa hawa wa gereza la Segerea. Mahitaji haya yalijumuisha vitu muhimu kama vile Sabuni, dippers za watoto, mafuta, nguo, na taulo za kike,n.k. Hii ikiwa ni msaada wa vitu kwa ajili ya matumizi mbalimbali katika maisha yao ya kila siku. Lengo la FINCA ni kuendelea kuigusa jamii na kuleta tabasamu kwa watu wenye changamoto na kuharakisha jitihada zao za kuboresha maisha yao. ...
News 15-05-2025
Kama sehemu ya kuunga juhudi za kuisaidia jamii inayoihudumia, FINCA Tanzania mapema mwaka huu ilishiriki Mbio za Kimataifa za Kilimanjaro za mwaka 2025. Kwa ushiriki huo FINCA ilichangia kampeni ya “Tumaini la maisha” ambapo waandaaji wa mbio hizo walitoa 5% ya kila ada ya ushiriki kusaidia matibabu ya watoto wanaougua saratani. Washiriki kutoka FINCA walivalia mavazi yenye nembo ya “FINCA Runners” ambayo pia ilisaidia kwa nembo ya FINCA kuonekana kwa zaidi ya washirki 20,000 katika mbio hizo. Pongezi za dhati kwa Afisa Mkuu wa Biashara, Felician Girambo, ambaye alipata medali kwa kumaliza mbio za kilomita 21 kwa wakati.
News 19-06-2024
Benki ya FINCA Tanzania inayo furaha kutangaza ufunguzi wa ofisi yake mpya huko Mafinga iliyoko karibu na soko la Mafinga. Mafinga ina idadi inayokua ya watu na muhimili wa kibiashara unaochipukia kwa kasi.
















