Mtoto Akaunti

Kuweka akiba kumerahisishwa kwa ajili ya mtoto wako

Anzisha msingi wa maisha ya baadae ya mtoto wako kwa njia rahisi ya kumuwekea akiba.

Hakuna makato

Anza kumuwekea mtoto wako akiba kwa maisha yake ya baadae kwa akaunti isiyo na makato ya wala gharama za uangalizi.

  • Gharama nafuu
    Furahia akaunti isiyo na makato ya kila mwezi. Kuweka pesa kwa wakala na kwenye matawi yetu ni bure.

  • Maandalizi ya baadae
    Msaidie mtoto wako kujiandaa na maisha ya baade na kumfunza kuhusu elimu ya kifedha mapema.

  • Akiba inayokuwa
    Akaunti hii ina riba itakayowezesha akiba ya mtoto wako kukua.

  • Kujifunza majukumu
    Akaunti hii unamfunza mtoto wako umuhimu wa kuweka akiba kwa ajili ya maisha ya baadae.

Ni rahisi kuanza kumwekea akiba

Anza safari rahisi ya kumwekea mwanao akiba kwa taratibu zetu rafiki na salam.

  • Fomu ya tamko la mzazi au mlezi
    Ni rahisi kufungua akaunti ya Mtoto kwa kujaza fomu ya tamko la mzazi au mlezi.

  • Kitambulisho cha kuzaliwa
    Rahisisha ufunguaji wa akaunti ya mtoto wako kwa kuonyesha kitambulisho chake cha kuzaliwa.

  • Kopi ya kitambulisho cha mzazi au mlezi
    Ambatanisha kopi ya kitambulisho chako ukiwa kama mzazi au mlezi.

Hatua kwa hatua namna ya kuanza maombi ya kujiwekea akiba

Kuanza maombi ya kujiwekea akiba tunazingatia uaminifu, ufanisi na nia ya kutimiza malengo yako ya baadae

  • 1

    Anza mchakato wa maombi
    Anza mchakato wa kufungua akaunti kwa kujaza fomu fupi hapa.

  • 2

    Utapigiwa simu kutoka kwa muhudumu wetu
    Utapigiwa simu na mtoa huduma wetu ndani ya masaa 24 kuhakiki baadhi ya taarifa.

  • 3

    Tembelea tawi
    Kamilisha mchakato wa kufungua akaunti ya mtoto wako kwa kutembelea tawi letu utakaloelekezwa na mtoa huduma wetu.

Anza maombi yako

Kuomba ni mchakato wa haraka na moja kwa moja.


Maswali yaulizwayo mara kwa mara

Mzazi au mlezi ajaze fomu ya tamko kutoka FINCA, cheti cha kuzaliwa cha mtoto na kopi ya kitambulisho cha mzazi au mlezi.

Mzazi yeyote au mlezi anaweza kufungua akaunti ya mtoto na kuweka akiba kwa niaba ya mtoto.

Mtu yeyote mwenye ukaribu na mtoto anaweza kuweka fedha.

Tunafurahi kuzungumza nawe

Weka namba yako ya simu tukupigie