WAMILIKI WA HISA WA DUNIA

FINCA Microfinance Bank ni kampuni tanzu ya sehemu ya FINCA Microfinance Holding Company LLC (FMH) yenye ubia wa uwekezaji unaowajibika kijamii (SRI) ambao unamiliki na kuendesha taasisi ndogo za fedha na benki 20 katika mabara matano. Wawekezaji wa FMH wanaongozwa na FINCA International Inc. Iliyiko Washington, D.C.-  isiyo ya kibishara na ndio yenye hisa nyingi za FMH. Wamiliki wa hisa wachache wa FMH ni International Finance Corporation (IFC), KfW, Nederlandse Financierings-Maatschappij voor Ontwikkelingslanden N.V. (FMO), Triple Jump na Triodos. FMH imeamua kutoa faida ya fedha kwa ajili ya uendelevu wa matumizi ya fedha na matokeo mazuri katika jamii.

IFC, mjumbe wa World Bank Group, ni taasisi kubwa sana ya maendeleo ya dunia inayolenga sekta binafsi. Inafanya kazi na kampuni binafsi katika nchi zaidi ya 100, wanatumia mtaji wao, utaalamu, na ushawishi kusaidia kutokomeza umaskini uliokithiri na kukuza ustawi wa pamoja. Katika FY13, uwekezaji wao uliongezeka kwa kiwango cha juu cha karibia bilioni, kutumia nguvu ya sekta binafsi kutengeneza ajira na kukabiliana na changamoto kubwa za maendeleo duniani.

Ilianzishwa mwaka 1948 kama taasisi ya sheria ya umma, KfWBankengruppe sasa inamilikiwa kwa 80% na Jamhuri ya Shirikisho ya Ujerumani na 20% inamilikiwa na serikali za shirikisho (“Länder”). Ikiwa na mizania yenye zaidi ya YURO bilioni 440, KfW ni moja kati ya benki zinazoongoza na zenye uzoefu mkubwa zaidi duniani. Kama benki isiyokuwa na mtandao wa matawi wala amana za wateja, inajigharamia biashara yake ya ukopeshaji kwa kutumia masoko ya mitajii ya kimataifa. KfWEntwicklungs bank ni sehemu ya KfWBankengruppe ambayo ni mshauri anayefaa na wa kimkakati kuhusu masuala ya sasa ya maendeleo. Kupunguza umaskini, kutafuata amani, kulinda maliasili, na kusaidia kuunda utandawazi ni vipaumbele vikuu vya  KfWEntwicklungsbank. Kwa niaba ya Serikali ya Shirikisho ya Ujerumani inafadhili mabadiliko, miundombinu na mifumo ya fedha kwa ajili ya kukua kwa  uchumi unaofaa kijamii na kiikolojia katika nchi zaidi ya 110. Ni mshirika wa fedha ulimwenguni na hutumia fedha zake katika miradi ya maendeleo.

Netherlands Development Finance Company (FMO ) ni benki ya maendeleo ya Kidachi. FMO inasaidia ukuaji endelevu wa sekta binafsi katika masoko yanayoendelea na yanayoibuka kwa kuwekeza kwa wajasiriamali wenye shauku. FMO inaamini sekta binafsi yenye nguvu inaongoza katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii, kuwawezesha watu kutumia ujuzi wao na kuboresha maisha yao. FMO inajikita katika sekta tatu ambazo zina matokeo makubwa katika maendeleo; taasisi za fedha, nishati na kilimo cha biashara, chakula & maji. Ikiwa na mtaji wa uwekezaji wa YURO bilioni 6.3, FMO ni mojawapo kati ya benki kubwa zaidi za maendeleo za sekta binafsi za Ulaya.

Dhamira ya TripleJump ni kuchangia katika maendeleo endelevu ya uchumi wa soko linaloibuka kwa kuwezesha uwekezaji katika biashara ndogondogo. Triple Jump inasaidia upanuzi wa taasisi ndogo za fedha zinazofaa katika hatua zote tatu za maendeleo (kuibuka, kupanuka na kukomaa) kwa kutoa mtaji na huduma za ushauri. Lengo lao ni kufanya kazi kwa matokeo mazuri ya kijamii katika masoko yanayoibuka kwa kuimarisha moyo wa ujasiriamali. Wanajikita katika MFIs ambazo zinajitolea kupunguza umaskini katika jamii yao, kuwafikia makundi ya wenye kipato kidogo na walioo katika mazingira magumu, hususan wanawake, kuiheshimu jamii na mazingira, na kufikia ufanisi mkubwa, uendelevu kifedha na kuzifikia jamii zilizo pembezoni.

Triodos Investment Management ni kampuni tanzu ya Triodos Bank kwa 100%, moja kati ya benki endelevu zinazoongoza duniani. Triodos Investment Management inafahamika kwa kuongoza duniani katika kuwezesha uwekezaji wenye manufaa kwa jamii, kusimamia uwekezaji wa moja kwa moja kuanzia katika miundombinu ya nishati endelevu hadi katika taasisi ndogo za fedha. Tangu mwaka 1994,  mali zake zikilizokuwa chini ya usimamizi katika huduma za fedha zimeongezeka hadi zaidi ya YURO milioni 500, kuifanya kuwa moja kati ya wawekezaji wanaoongoza katika tasnia. Kupitia mfuko maalumu wa fedha kwa sasa inatoa fedha zote za mkopo na hisa kwa taasisi za fedha 104 zinazoinukia pamoja na zilizoimarishwa vizuri katika nchi 44. Wanamiliki hisa sawa katika taasisi za fedha 21; wafanyakazi waandamizi wa Triodos Bank wanaingia wanaunda Bodi ya Wakurugenzi na wanachangia kikamilifu katika usimamizi wa taasisi hizi.