Mapema leo jumatatu tarehe 11/12/2023, Mkuu wa kitengo cha biashara benki ya FINCA Bwana Felician Girambo amekutana na kufanya mazungumzo na Umoja wa Wamiliki wa Shule Binafsi mkoani Arusha nia ikiwa kujenga mahusiano mazuri ya kibiashara baina yao na benki ya FINCA.

Bwana Girambo amewafahamisha wamiliki na viongozi wa shule binafsi kuhusu huduma na bidhaa mbalimbali zinazotolewa na benki ya FINCA ikiwamo mkopo wa wamiliki wa shule ambao umepunguzwa riba na wenye utaratibu mzuri wa marejesho.

Kwa upande wao wamiliki wa shule binafsi wameahidi kufikisha ujumbe huu mzuri wa FINCA kwa wamilki wenzao pamoja na wazazi kwa ajili ya kukopa mkopo wa ada ya shule wenye riba nafuu na utaratibu rahisi kuupata.